Saturday, July 4, 2015

PATAKATIFU

 UCHAGUZI MKUU 2015
"ukichaguliwa uwaambie ndugu zako na marafiki zako wote kabisa, Ikulu ni mahali patakatifu. Mimi sikuchaguliwa na wananchi wa Tanzania kuja kupageuza kuwa pango la walanguzi."{Mwalimu Julius Kambarage Nyerere}
Utakatifu wa Ikulu kwa Baba wa Taifa ulianza mapema kabla hata hajazoea kukaa katika jengo hilo. Kwake yeye, aliona Ikulu ni eneo muhimu kwa utambulisho na utakatifu wa maamuzi ya kila siku kwa taifa. Kutokana na chuki ya Baba wa Taifa kwa ukoloni na wakoloni, alifikia hata kukejeli jumba hilo kwa kuwa lilikaliwa na wakoloni.
Kwa ufahamu na heshima yake kwa kitu kinachoitwa Ikulu, alipata shida sana kuona mtu anawezaje kuishi ikulu kisha akakandamiza, akahujumu uchumi, akaiba, akadanganya, akatukana, akafanya usanii, akafanya uhuni, akadhulumu, akapotosha, akaringia wananchi, akafanya biashara, akapigana na mkewe, au hata kupageuza Ikulu kuwa eneo la kufugia, kutunza ukoo wake na mambo mengine binafsi. Kwake Baba wa Taifa, Ikulu yalikuwa ni madhabahu ya taifa letu, mahali pa kuheshimiwa na kuogopwa
Haikushangaza wengi, miaka michache baada ya uhuru, Baba wa Taifa alianza jitihada za kuhama Ikulu na kuishi katika nyumba yake binafsi iliyo Msasani. Alifanya hivyo si kwa sababu aliidharau Ikulu ya Magogoni, bali alikuwa anajilinda ili asiingie katika majaribu ya kuigeuza Ikulu kuwa ni nyumba ya ukoo wa Burito.
Aliona Ikulu ni ofisi na alikwenda kazini kama Watanzania wengine, kisha alirudi kulala Msasani katika nyumba aliyojenga mwenyewe kwa mkopo ambao alishindwa hata kuulipa na kukaribia kunyang’anywa.
Kutokana na hofu iliyoambatana na heshima kwa Ikulu yetu, Baba wa Taifa aliona Ikulu pawe ni mahali pa kukaribisha wageni wa kitaifa, kufanya shughuli za ofisi na kufanyia maamuzi muhimu ya kitaifa. Alijua yeye kama mwanadamu anaweza kuwa na hulka zisizohitajika na kuingilia maslahi ya taifa letu.
Hakuwa na maana kuwa marais watakaofuata wasiishi Ikulu kama yeye, bali alilenga kuonyesha eneo lile liwe zaidi ya pango la kuishi wanadamu wenye kutanguliza maslahi yao, familia zao na marafiki zao. Haishangazi kuona leo watu wanahasimiana kutaka kwenda kuishi katika jengo hilo la kikoloni.
Ukiiangalia Ikulu ya Baba wa Taifa na Ikulu yetu ya leo ni kama tuna Tanzania mbili. Ukiacha mengi yanayoweza kujadiliwa kwa nafasi yake, hili la matamko yanayotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano yanaacha maswali mengi na sononeko la mioyo kwa Watanzania wengi wanaoiheshimu Ikulu yetu.
JAJI Warioba Mtu wa Watu.'s photo.
 

No comments:

Post a Comment